Taarifa kutoka kwa waangalizi wa uchaguzi (Coalition on Election Monitoring and Observation in Tanzania)

CEMOT logo

Utangulizi

Kituo cha uangalizi wa uchaguzi kinakusanya taarifa za mchakato wa uchaguzi kutoka nchi nzima. Kwa kutumia teknolojia ya kisasa, waangalizi wetu zaidi ya mia tatu wanawasilisha taarifa zinazotuwezesha kutambua mwenendo wa uchaguzi, matukio ya pekee na madhara yanayoweza kutokana na matukio hayo. Waangalizi wetu wamesambaa katika majimbo yote 265 Tanzania Bara na Zanzibar ambapo wanatutumia taarifa kila siku.

Waangalizi wetu wanafuatilia mikutano miwili kila siku inayoweza kuwa ya wabunge, madiwani au urais. Taarifa zinazokusanywa zinajikita kwenye maeneo makuu sita ambayo ni mwenendo wa vyama siasa, utendaji kazi wa Tume za uchaguzi, uwepo na utendajo wa jeshi la polizi, ushiriki wa makundi maalumu, usalama na elimu ya mpiga kura. Kwa siku mbili zilizopita, waangalizi wetu wametembelea vituo mbalimbali vya kupiga kura, kushuhudia maandalizi ya uchaguzi.

Uchambuzi huu unatokana na taarifa tulizozipokea kutoka 25/9/2015 and 24/10/2015, kutoka kwa waangalizi 301 katika majimbo 229 Tanzania bara na Zanzibar.

.

 1. Mikutano ya kampeni iliyoangaliwa na waangalizi

 

241015 campaign meetings

241015 campaign meetings 2

.

 1. Elimu ya mpigakura

241015 voter education

Ripoti za waangalizi zinaonesha ongezeko la elimu ya mpigakura kadri uchaguzi unavyokaribia.

.

 1. Ushiriki wa wanawake na vijana

241015 wagombea wanawake 2010 2015

Kwa kasi hii, itachukua uchaguzi 31 hadi idadi ya wagombea ubunge wanawake iwe sawa na idadi ya wanaume. Hii ni zaidi ya miaka 150.

241015 wagombea wanawake by party

 • Asilimia 9 ya wagombea ubunge wa CCM ni wanawake
 • Asilimia 6 ya wagombea ubunge wa CHADEMA ni wanawake
 • Asilimia 15 ya wagombea ubunge wa ACT-Wazalendo ni wanawake
 • Asilimia 11 ya wagombea ubunge wa CUF ni wanawake
 • Kundi lenye wagombea ubunge wengi wanawake ni vyama vingine vilivyosalia

 

241015 registered voters by gender 241015 registered voters by age group

 • Zaidi ya nusu ya wapigakura walioandikishwa ni wanawake (53%)
 • Zaidi ya nusu ya walioandikishwa na NEC ni vijana chini ya miaka 35

.

 1. Udhalilishaji wa wanawake wakati wa kampeni

Takwimu hizi zinatokana na ripoti za waangalizi 196, waliotuma ripoti kati ya tarehe 19 na 24 Oktoba:

241015 gender discrimination

Kuna ripoti chache tu za unyanyasaji wa kijinsia wakati wa kampeni, katika siku sita za uangalizi.

.

 1. Vyama kutii / kutotii kanuni na taratibu za kampeni

241015 breaches of rules by parties

Ripoti za waangalizi zinaonesha kwamba hakuna mabadiliko katika kutii au kutotii miongozo na taratibu za uchaguzi kwa upande wa vyama.

.

 1. Maandalizi ya NEC

241015 NEC preparedness

Idadi ya ripoti za waangalizi zinazoashiria kukamilika kwa maandalizi ya uchaguzi zinazidi kuongezeka.

.

Hitimisho

Kwa ujumla, taarifa hizi zinaonesha kwamba nchi yetu ipo tayari kwa uchaguzi, ingawa kumekuwa na changamoto za hapa na pale.

Tunahimiza Watanzania watumie haki yao ya kupiga kura, na tunaitakia nchi yetu uchaguzi mwema.